Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joao Felix anukia Arsenal

Joao Felix.jpeg Joao Felix anukia Arsenal

Thu, 24 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ARSENAL imetajwa kumuwania saini ya nyota wa Atletico Madrid, Joao Felix na kocha Mikel Arteta akitajwa kuwa na mpango naye Felix alijiunga na Atletico Madrid mwaka 2019 kwa pauni 113m kutoka Benfica ameshindwa kutamba kikosini hapo.

Inaelezwa kuwa majira ya joto mwaka huu kuna uwezekanao mkubwa kwa Felix kuondoka kikosini hapo na Atletico wakamsajili Concalo Guedes wa Valencia kama mbadala wake.

Ripoti zinaeleza kuwa Arsenal tayari wameanza kumfuatilia kwa ukaribu Mreno huyo hasa baada ya kumkosa Dusan Vlahhovic, Januari mwaka huu, Felix bado ana mkataba wa miaka minne na Atletico na kipengele cha kutaka kumuachia ni kiasi cha pauni 219m.

Imeelezwa kuwa Arteta anataka kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji licha ya Felix hivi karibuni kiwango chake kuonekana kusuasusa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live