Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joan Laporta: Haikuwa Rahisi Kumpata Xavi

Xavi Hernandez Laporta Can Fix Everything At Barca.jpeg Joan Laporta akiwa na Xavi Hernandez

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameweka wazi kuwa haikuwa kazi rahisi kukamilisha uhamisho wa kocha wao mpya Xavi Hernandez kutoka kwenye klabu ya Al Sadd hasa kwenye kipindi hichi cha ukata wanachopitia.

Joan Laporta hakusafiri kwenda jijini Doha kufanya makubaliano na klabu ya Al Sadd kwenye uhamisho wa Xavi badala yake aliwatuma Mateu Alemany na Rafa Yuste kufanikisha uhamisho huo.

Uhamisho huo umechukua muda kukamilikia kutokana na ukata ambao klabu ya Barcelona inapitia, hadi kufikia hatua ya kumshawishi Xavi mwenye atoe kiasi fulani cha fedha ili kufanikisha uhamisho huo, Barcelona haikuweza kufanikiwa kuvunja mkataba ambao ulikuwa na thamani ya pauni milioni 5 peke yake.

Rais wa Barcelona Joan Laporta hakuweza kutoa maelezo kwenye utambulisho wa xavi, “kufanikisha kuondoka al sadd, klabu na xavi walishirikiana kuwa kitu kimoja na tumefanikiwa, haya ni maelezo kwa kifupi.” Alisema Laporta

Xavi sasa ni kocha rasmi wa klabu ya Barcelona na ameshepewa mikoba ya kuiondoa nafasi ya tisa kurudi kwenye ushindani wake na kuhakikisha kuwa anaivusha kwenye klabu bingwa barani ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live