Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joan Laporta: De Jong alikuwa muhimu kubaki kwetu

Frankie De Jong 1 1536x889 Kiungo wa Barcelona, De Jong

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesema walihitaji kumbakiza kiungo wao raia wa Uholanzi Frenkie de Jong baada ya kuhitajika na vilabu kadhaa.

Laporta ameeleza walipokea ofa nyingi kutoka katika timu nyingi nchini Uingereza ila wao lengo lao zaidi ilikua ni kumbakiza mchezaji mwenye ubora kama De Jong.

“Tulipokea ofa nyingi kutoka timu za Uingereza tena hela kubwa, Ila tuliamua kumbakiza mchezaji mwenye ubora wa Frenkie”

Kuna taarifa pia kua klabu ya Barcelona walikua wakilazimisha wachezaji wake kupunguza mishahara ili kuendana na matumizi ya klabu ila Rais huyo amekataa hizo tuhuma

“Hatujawahi kulazimisha mchezaji kupunguza mshahara, Tuliuliza katika njia nzuri tu” Alisema Joan Laporta

De Jong mchezaji ambae alihitajika zaidi na klabu ya Manchester United kwa kipindi chote cha majira ya joto na aliamua kubakia katika klabu ya Barcelona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live