Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinsi Saudia itakavyokomba mastaa Ulaya

Messi Return Jinsi Saudia itakavyokomba mastaa Ulaya

Sat, 13 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Dirisha la majira ya kiangazi linazidi kunukia. Huu ndio wakati ambao inaaminika kwamba timu nyingi zinatumia sana pesa kwenye kujenga vikosi vyao.

Hata hivyo hivi karibuni kumekuwa na utawala mpya wa waarabu kuanzia kwenye umiliki wa timu hadi kusajili wachezjai wenye majina makubwa kama ilivyofanya Al Nassr kwa Cristiano Ronaldo.

Kuelekea dirisha lijalo pia kuna majina mengi makubwa yanatarajiwa kutua Uarabuni hususani Saudi Arabia na hapa tumekuchambulia kwa kina baadhi ya mastaa hao wanaoweza kutua nchini Saudia. Lionel Messi

Ni jina linalotajwa zaidi. Lionel Messi anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo mkataba wake na PSG utakuwa umemalizika.

Messi ambaye mahusiano yake na timu hiyo yamevurugika katika siku za hivi karibuni anadaiwa kuwa anawindwa na timu nyingi nchini Saudia huku inayoonekana kuwa na nguvu zaidi ni Al Hilal ambayo ipo tayari kutoa Pauni 320 milioni kwa mwaka kama mshahara ili kumsajili.

Mbali ya pesa hizo nyingi kutoka Saudi Arabia, Barcelona pia inahusishwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kumrudisha lakini changamoto kubwa inaonekana ni kuwa kiasi cha pesa ambacho waarabu wamekiweka.

Sergio Busquets

Ili kufanya usajili wa wachezaji mbali mbali katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi mabosi wa Barca wanataka kuachana na baadhi ya wachezaji na mmoja wao ni huyu Busquets.

Barca ilitaka kumbakisha staa huyu lakini kwa sharti la kumpunguzia mshahara jambo ambalo alilikataa.

Kama iliyvyo kwa Messi fundi huyu pia yupo kwenye rada za Al-Hilal ya Saudia ambayo kwa taarifa zilizochapishwa na gazeti la Mundo Deportivo ipo tayari kumlipa Pauni 300,000 kwa wiki.

Wilfried Zaha

Mkataba wa sasa Zaha unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na mkataba wowote atakaousaini baada ya hapa ndio itakuwa fainali yake ya uzeeni kwani kwa sasa ana umri wa miaka 30.

Winga huyu wa kimataifa wa Ivory Coast mwenyewe ameonyesha zaidi nia ya kutaka kujiunga na timu itakayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa ingawa uwepo wa timu kutoka Saudia huenda ukabadilisha mawazo yake.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail, Zaha amepokea ofa Pauni 173,000 kwa wiki kutoka Al-Ittihad wakati huo Palace yenyewe imepanga kumpa ofa ya mkataba mpya wa Pauni 200,000 kwa wiki.

Hugo Lloris

Lloris anatarajiwa kuondoka katika kikosi cha Tottenham mwisho wa msimu huu. Kipa huyu wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 37, hayupo kwenye mipango ya timu hiyo kwa msimu ujao na tayari waarabu wanataka kumpa mshahara mara tatu ya ule anaupokea hivi sasa.

Lloris ambaye aliwahi kushinda kombe la Dunia akiwa na Ufaransa mwaka 2018, mshahara wake wa sasa ni Pauni 100,000 kwa wiki, hivyo utaongezeka hadi kufikia Pauni 300,000.

Jordi Alba

Moja ya mpango wa Al-Hilal ni kuhakikisha Alba anacheza pamoja na Messi na Busquets.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 34, bado ana miezi 13 iliyobakia kwenye mkatababwake wa sasa lakini naye ni mmoja ua mastaa wanaotakiwa kuuzwa mwisho wa msimu huu kutokana na kiwango chake.

Hijafahamika hadi sasa ni kiasi gani Al-Hilal inataka kumlipa ingawa inaaminika kuwa huenda akapewa ofa sawa na ile ya Busquets.

N'Golo Kante

Kante anajulikana kama mmoja kati ya viungo wakabaji hatari zaidi kuwahi kutokea nchini England ingawa majeraha ya mara kwa mara yamepunguza sana ufanini wake tangu kuanza kwa msimu huu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Foot Mercato, timu ya sasa ya Ronaldo Al-Nassr imeonyesha nia ya kutaka kumsajili ingawa upinzani umekuwa mkubwa sana kutoka kwa Barcelona na Chelsea yenyewe ambazo zote zinapambana kumbakisha Ulaya.

Hata hivyo mpunga ambao wataweza ndio unaweza kuamua hatma ya mwamba huyu. Roberto Firmino. Alishatangaza kwamba ataondoka Liverpool itakapofika mwisho wa msimu lakini swali ni je? atajiunga na timu gani.

Kumekuwa na tetesi ya kwamba timu za Italia zinamtamani sana lakini pia kumekuwa na uvumi wa timu za Saudia kutaka kumsajili.

Dili linaonekana kuelemea zaidi upande wa timu hizi za saudia kwa sababu kwa namna yoyote timu za Italia kutokana na uchumi wao wa sasa ni ngumu sana kutunishiana misuli ya kifedha na mabosi wa kiarabu.

Chanzo: Mwanaspoti