Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinamizi la penalti lamkaba Gabaski

Mohamed Abou Gabal Gabaski Jinamizi la penalti lamkaba Gabaski

Sat, 3 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Inaonekana maluweluwe ya kukosa penalti katika mechi ya 16-Bora yanaendelea kumuandama kipa wa Misri, Mohamed Abou Gabal ‘Gabaski’ ambaye sasa amejitokeza kuomba radhi.

Misri ilitupwa nje ya michuano ya Afcon 2023 baada ya kuwa na mwendo wa kufadhaisha wakishindwa kupata ushindi hata mmoja ndani ya dakika 90 za mchezo.

Mafarao hao waliambulia sare tatu mfululizo za mabao 2-2 katika hatua ya makundi dhidi ya Msumbiji, Ghana, na Cape Verde kabla ya kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya DR Congo katika hatua ya 16-Bora.

Wakati mechi ilipoingia katika kupigiana matuta, alikuwa ni Gabaski aliyekosa yake na kuwaruhusu DR Congo kushinda kwa penalti.

Zilikuwa ni siku chache mbaya kwa Gabaski ambaye alikosa penalti timu yake ya Misri ikitolewa mapema Afcon, huku pia dili lake la uhamisho wa kwenda kujiunga na klabu bingwa ya Afrika, Al Ahly nalo likafeli.

Alipoulizwa kuhusu kukwama kwa uhamisho wake wa kujiunga na Al Ahly kutolewa Afcon, Gabaski alisema: “Mijadala yote inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii haihusiani kwa namna yoyote na mimi, nami nimeendelea na msimamo wa kubaki kimya.

“Ninayopitia kwa sasa yananitosha; baada ya kutolewa Mataifa ya Afrika, napitia hali ambayo sio rahisi kuishi ndani yake, na haya ni mazingira magumu sana.

“Tunaomba radhi kwa watu wote wa Misri kwa kutolewa kwetu kwenye Mataifa ya Afrika. Tulitarajia kufuzu fainali kwa sababu watu wa Misri wanastahili hilo.

“Inshaallah, tutarekebisha makosa yetu na tutakuwa bora zaidi siku zijazo. Michuano ijayo itakuwa yetu. Tumeshindwa kutimiliza majukumu yetu kwa namna fulani na tumeshindwa kufikia malengo yetu, kwa sababu dhamira yetu ilikuwa ni kutwaa ubingwa.”

Chanzo: Mwanaspoti