Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinamizi la mafua laitesa Ufaransa

Ufaransa Hmk.jpeg Jinamizi la mafua laitesa Ufaransa

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kirusi cha mafua, kuumwa koo na homa kinaendelea kusambaa kwenye kikosi cha Ufaransa. Shirikisho la soka la Ufaransa limethibitisha.

Ugonjwa huo ulianza na Adrien Rabiot na Dayot Upamecano, wawili hao hawakuweza kucheza mechi ya nusu fainali dhidi ya Morocco.

Baada ya hao, alifuatia Kingsley Coman na sasa ni Raphael Varane na Ibrahima Konate ambao wanaumwa na wameshindwa kuhudhuria mazoezi.

Mshambuliaji Randal Kolo Muani amesema kuwa wachezaji wanaoumwa wametengwa kwenye vyumba na wanapatiwa huduma nzuri na madaktari. Tumewekewa sheria kali ya kutokaribiana.

Naye kocha Didier Deschamps amesema anatarajia Upamecano na Radiot watakuwa fiti kabisa kufikia mechi ya fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live