Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jinamizi la Mbappe laitesa Real Madrid

Kylian Mbappe Fiert Win Kylian Mbappe

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Real Madeid, Dani Carvajal amekiri wachezaji wenzake walidhani Kylian Mbappe angejiunga nao katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Straika huyo wa Paris Saint-Germain alihusishwa na Madrid baada ya kugoma kusaini mkataba mpya PSG, lakini alibaki.

Lakini kwa mujibu wa beki huyo, waliona kila dalili kwamba Mfaransa huyo angetua Santiago Bernabeu baada ya kujadili na wenzake.

Carvajal alisema: “Siwezi kudanganya kwamba hatukujadili, lakini wakati tupo katika ziara Marekani maneno mengi yalizungumzwa. Nilidhani angejiunga (Madrid) na nilijua Mbappe angechagua timu yetu.

Baada ya kukosa ziara ya PSG niliamini anatua kwetu, lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia.”

Mbappe alitatua mzozo na mabosi wake PSG ambao ulidumu muda mrefu bila kupata muafaka kuhusu hatima yake.Taarifa zilidai angesaini mkataba mpya PSG utakaodumu hadi 2026.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live