Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jezi za Yanga CAF kuanza kuuzwa kesho

Yanga Jezi Mdg Jezi ya Kimataifa ya Yanga kuanza kuuzwa kesho

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Young Africans imetangaza kuwa itaanza kuuza jezi zake maalumu kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kesho saa 8:00 mchana Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani Jijini Dar Es Salaam.

Taarifa ya idara ya habari na mawasiliano kwa umma ya klabu hiyo imebainisha kuwa awali, jezi hizo zilikuwa zianze kuuzwa leo Novemba 30, 2023 lakini kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza, zoezi la uuzaji litafanyika kesho Desemba 1, 2023.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na unawaalika wote kesho mchana Makao Makuu ya Klabu kujipatia jezi hizi namba moja kwa ubora Barani Afrika.” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: