Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jezi ya Maradona yarejea Argentina

 127271779 1fb970068d2e0f21b2630c6b27d20f8219d19e310 0 5472 36481000x667.jpeg Jezi ya Maradona yarejea Argentina

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Argentina na zaidi wapenzi wa soka nchini humo wanasheherekea kurudi kwa jezi ya mkongwe wa soka Diego Maradona. Jezi hiyo iliwasili Jumatano wiki hii.

Miaka 36 baada ya Argentina kuitoa Germany kwenye fainali za kombe la dunia 1986, jezi ambayo Maradona aliivaa katika kipindi cha kwanza cha mechi imekabidhiwa rasmi kwa Shirikisho la soka la Argentina (AFA).

Kiungo wa zamani wa Germany Lothar Matthaus ambaye alibadilishana jezi na Maradona wakati wa mapumziko, amesema kuwa ameamua kujitolea jezi hiyo kwa watu wa Argentina.

Matthaus aliikabidhi jezi hiyo katika hafla iliyofanyika katika ubalozi wa Argentina nchini Hispania mwezi Agosti na hatimaye jezi hiyo imewasili Argentina.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live