Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeuri ya Zahera ni Kakolanya TU

33690 Kakolanya+pic Tanzania Web Photo

Thu, 27 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

HUWEZI kuamini, ila ndivyo ukweli ulivyo kuwa, licha ya figisu zinazoenda na kipa Beno Kakolanya, Kocha Mwinyi Zahera anakiri kipa huyo ni mmoja kati ya wachezaji waliopa jeuri katika Ligi Kuu Bara wakiwa vinara mbele ya Azam Fc na Simba.

Kakolanya na Zahera wametibuana hivi karibuni baada ya kipa huyo kususia mazoezi kama shinikizo la kupata kulipwa fedha anazoidai klabu hiyo na kocha huyo kukataa kumpokea baada ya kujisalimisha hivi karibuni.

Wakati ishu yake ikiendelea kujadiliwa ili kipa huyo arejeshwe kikosini, Mkongo huyo aliyekuwa Ufaransa ameshindwa kujizuia kwa kuwamwagia sifa nyota wake wanaompa kiburi na kuzidi kukaa kilele mwa Ligi Kuu, huku akimtaja pia Kakolanya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Zahera aliyeingia mkataba wa kuinoa timu hiyo Mei 18 mwaka huu, alifichua tangu ajiunge na Yanga na kuisaidia kufika hapo ilipo kwa sasa ni sababu ya nyota wake akiwamo Kakolanya, japo ameshindwa kuwa naye kikosini kwa sasa.

Zahera alisema kipa huyo aliamini ndiye atakayekuwa mfano kwa chipukizi imekuwa tofauti na ameweza kuonyesha picha mbaya na kushindwa kuivumilia timu kutokana na hali mbaya iliyokuwepo kiasi cha kumng’oa kwenye mipango yake kwa sasa. Zahera alisema kumtaja Beno haina maana amemsamehe kile alichokifanya, ila amemtaja kwa vile anatambua uwezo wake ndani ya uwanja na ni mmoja ya nyota wake wa kikosi cha kwanza anachojivunia.

Mbali na Kakolanya, Zahera amewataja wengine kuwa ni; Paul Godfrey, Gadiel Michael, Andrew Vicent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Papy Kabamba Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Heritier Makambo, Ibrahim Ajibu na Deus Kaseke.

Zahera alisema hao ndio nyota wake ambao amekuwa akiwatumia mara kwa mara na wamekuwa wakimpa matokeo japo kuna wengine wamekuwa wakitokea benchi na kusaidia timu kupata matokeo.

“Yanga ina nyota wengi wazuri na wanaopenda mafanikio, ila inaniwia vigumu kukaa nao kuwapa elimu kuwa soka linachezwa uwanjani ili waweze kurudi katika mstari na kuondokana na unyonge wao wa madai waliyonayo kwa viongozi nimelifanikisha hilo kwa kiasi kikubwa ni Beno tu ambaye ameshindwa kuonyesha uungwana,” alisema.

“Nimewataja nyota hao kwa vile nimekuwa nikiwatumia mara kwa mara sina maana niliowaacha hawana msaada kwa timu kila mmoja anaweza na ndio maana kasajiliwa na muda mwingi nimekuwa nikitoa nafasi kwa kila mchezaji hivyo kupambana kwao ndio kutawapa nafasi ya kuwa katika kikosi cha kwanza,” alifafanua Zahera.

Aliongeza, kikosi hicho kimeweza kufanya vizuri kikiwa katika hali mbaya ya kiuchumi kimepambana kwa kila hali jambo ambalo hana budi kukipongeza na anaamini kitaendeleza mapambano hadi kufikia mafanikio ya kutwaa ubingwa msimu huu.



Chanzo: mwananchi.co.tz