Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jesus azua hofu Arsenal, kukaa nje miezi mitatu

WhatsApp Image 2022 12 07 At 09.jpeg Gabriel Jesus aliumia katika mchezo dhidi ya Cameroon

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Arsenal na Timu ya Taifa ya Brazil, Gabriel Jesus amefanyiwa upasuaji wa goti lake alilopata jeraha katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Cameroon.

Jesus alishindwa kumaliza mchezo huo na kulazimika kutolewa nje huku taarifa zikisema halikuwa jeraha kubwa.

Sasa taarifa rasmi kutoka katika klabu ya Arsenal imethibitisha kuwa Mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa majuma kadhaa akiendelea kuuguza jeraha lake taratibu kabla ya kurudi Dimbani.

Kuumia kwa Jesus ni pigo kubwa kwa Mwalimu Mikel Arteta na Timu ya Arsenal kwa ujumla katika kampeni ya kusaka taji la EPL.

Arsenal mpaka sasa wanaongoza msimamo wa EPL na Jesus amekuwa chachu ya mafanikio hayo kabla ya Ligi nyingi Barani Ulaya kusimama kupisha michuano ya Kombe la Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live