Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jesse Lingard atalazimisha kuondoka United

Featured Image 12 1024x683 1 Jesse Lingard

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jesse Lingard amesisitiza kuwa anataka kuondoka baada ya mazungumzo na klabu ya Manchester United ya mkataba mpya kushindikana.

Jesse Lingard alikataa mkataba alioandaliwa na klabu ya Man United mwezi oktoba, ambao ulikuwa na thamani ndogo kuliko aliokuwa nao sasa hivi na kwa sasa hana mpango wa kufungua milango kwa mazungumzo mengine na miamba ya Old Traford.

Lingard anatarajia kutolewa kwa mkopo baada ya kupata nafasi chache, tokea kuwasili kwa Ronaldo kwenye viunga vya Carrington Park licha kuonyesha kiwango kikubwa alipotolewa kwa mkopo kwenda klabu ya West Ham.

Jesse Lingard baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kushindikana anatarajia kuondoka kama mchezaji huru majira ya kiangazi mwakani, huku klabu kadhaa kubwa zimeonesha nia ya kuhitaji huduma yake Barcelona na Ac Milan zimekuwa mstari wa mbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live