Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Jeshi la Wananchi' 60 kuifuata Al Ahly

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga.

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Yanga, kinatarajiwa kuanza safari leo kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Yanga na Ahly ambao wote wameshafuzu hatua ya robo fainali, watakipiga kwenye mchezo huo unaotarajiwa kufanyika Ijumaa, Machi 1, 2024 majira ya saa 1:00 nchini Misri.

“Timu itafikia Hotel ya Royal Kempisc ambayo ni hoteli yenye hadhi ya nyota tano.

“Tutaondoka na msafara wa watu 60 kutoka Dar kwenda Cairo. Msafara huo umegawanyika kwenye mafungu matatu, fungu la kwanza ni wachezaji ambao watakuwa wachezaji 24, majina ya wachezaji tutawajuza kwenye platform zetu.

“Kundi la pili ni technical staffs ambao watakuwa 13, ambao wataungana na wachezaji wetu, officials kwa maana ya viongozi watakuwa 23. Yupo Rais wa Klabu Eng. Hersi Said, watendaji wa klabu, Mkuu wa Msafara kutoka TFF ambaye ni Makamu wa rais, mzee Athuman Nyamlani na baadhi ya wanachama waandamaizi.

“Mchezo huu utapigwa Ijumaa, Machi 1, 2024 majira ya saa 1:00 jioni kwa majira ya hapa kwetu Tanzania," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live