Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Gamondi kamili gado kuwavaa Simba

Yanga 699 1024x627.jpeg Jeshi la Gamondi kamili gado kuwavaa Simba

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo majira ya saa 11:00 jioni, kikosi cha Young Africans SC kitashuka dimbani kumenyana na Simba ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili, utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku sisi Yabga wakiwa wenyeji.

Young Africans SC leo wanaingia uwanjani wakiwa kifua mbele kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza ambao walishinda magoli 5-1 dhidi ya Simba, huku kwa sasa wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi 55 baada ya mechi 21.

Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi, amesema: “Kitu muhimu kwetu ni kushinda mechi hii kwa ajili ya kuendelea kuwania ubingwa, ninaziheshimu timu zote, tunapambana kushinda mechi zetu, tutaona nini kitatokea, lakini malengo yetu ni kushinda na kuwapa furaha Wananchi.

“Tunajaribu kufanya tuwezavyo, kitu muhimu kwangu ni kuiendeleza hali yetu ya kushinda.”

Dabi hii imekabidhiwa kwa wazee wa Young Africans na kupewa jina la Wazee Day.

Kutokana na hilo, Nahodha Msaidizi wa Young Africans SC, Dickson Job, amesema: “Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri, tunaamini mchezo utakuwa mgumu na wenye upinzani, lakini kikubwa sisi kupambana na kupata matokeo mazuri katika mchezo huo.”

Kuhusu Wazee Day, Job amesema: “Ni kitu kizuri kwa sababu ukizingatia hii timu ni timu ya watu na timu ya Wananchi na wapo wazee, kwa hiyo tupo tayari kuwapambania wazee wetu na kuendelea kuwapa heshima kwa sababu ni watu wanaoipambania sana timu yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live