Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeshi la Azam FC kuanza safari ya kuivamia Libya

Azam FC KIKOSI MBEYA 1140x640 Kikosi cha Azam FC

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Kikosi cha Azam FC kesho Alhamis (Oktoba 06) kitaanza safari ya kuelekea Libya tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi Al Akhdar.

Azam FC imethibitisha kuwa msafara wa kuelekea Benghazi-Libya utakuwa na wachezaji wetu 25, huku safari ikitarajiwa kuwa saa 11.25 Alfajiri.

Mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza umepangwa kupigwa Jumamosi (Oktoba 08) saa 2.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Chanzo: dar24.com