Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeremiah Juma alia na upepo

Jeremia Juma Jeremiah Juma alia na upepo

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Jeremiah Juma amesema upepo mbaya umempitia katika michezo mitano ya Ligi Kuu Bara akashindwa kupachika bao hata moja, lakini anaamini wenzake wanafanya kazi kubwa.

Juma, mshambuliaji tegemeo wa klabu hiyo ya Wajelajela msimu huu hajauanza vizuri tofauti na uliopita kwani katika michezo mitano alikuwa na mabao mawili.

Alisema kutofunga ni upepo tu umepita, lakini anaamini muda huu ambao ligi imesimama ataendelea kujiweka sawa kuhakikisha anafunga.

“Mpira wakati mwingine unabadilika hakuna mchezaji ambaye hataki kufunga ni mambo tu yanakwenda ndivyo sivyo, lakini naamini nitaanza kufunga,” alisema.

Juma alikiri kwamba upinzani mkubwa wa ligi uliokuwepo na wenyewe ni moja ya chachu ya timu kutofanya vizuri, lakini ndio upinzani unavyotakiwa kuwepo.

“Sasa hivi hakuna cha nyumbani wala ugenini popote pale timu inapata matokeo au inapoteza. Hiyo inaonyesha namna ambavyo timu zimejipanga na kuleta ushindani ambao unaifanya ligi yetu inazidi kuwa bora,” alisema mchezaji huyo.

Alisema wanao mchezo wa nyumbani dhidi ya JKT Tanzania ligi itakaporejea na baada ya hapo wataifuata KMC jijini Dar es Salaam.

“Hakuna mchezo rahisi hata kidogo zamani timu chache ndizo zilikuwa zikiogopwa ila sasa hivi yoyote ile ukizubaa unachapika (mabao),” alisema mchezaji huyo.

Chanzo: Mwanaspoti