Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jeremia kisubi, Kibu Denis bado wingu zito Msimbazi

Pjimage (3) Mlinda mlango Jeremiah Kisubi (mwenye fulana nyeupe) na kibu Dennis

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Picha zimeonekana za wachezaji wa Simba wakiwa kwenye Mazoezi kule Jijini Arusha ikiwa ni maandalizi kujiwinda na msimu mpya 2021/2022.

Katika Picha hizo wameonekana wachezaji wawili ambao wamezungumzwa sana kujiunga na simba msimu huu, Jeremia Kisubi na Kibu Dennis, Mshambuliaji kutoka klabu ya Mbeya City kutoka kule Jijini Mbeya.

Wachezaji hao wameonekana wamevaa jezi za Simba, wakiendelea kujifua 'Gym" na wachezaji wengine wa Simba.

Jambo lililozua maswali mengi kwa kuwa Simba imetambulisha wachezaji wake wote iliyowasajili dirisha hili.

Mratibu wa Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC, Abbas Ally alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema;

"Sina taarifa kama ni wachezaji wa Simba kwa sababu wachezaji wa Simba wote tulishawatambulisha kwa mashabiki,lakini suala la kuvaa jezi hawa ni wachezaji hivyo mara nyingi mwisho wa mechi huwa wanabadilishana jezi kwa hiyo je kama kapenda tu kuivaa"

Aidha Uongozi kutoka ndani ya Klabu ya Mbeya City umethibitisha kuwa mchezaji Kibu Dennis sio mali yao na walishamaliza mkataba baina yao kama klabu na mchezaji.

Kwa Upande wa Golikipa kutoka Prisons,Jeremiah Kisubi uongozi wa Klabu ya Prisons ulishatamka kuwa ni miongoni mwa wachezaji walioondoka ndani ya kikosi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live