Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la Yanga lanusurika kubomolewa

Jengo La Yanga Lanusurika Kubomolewa Jengo la Yanga lanusurika kubomolewa

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema jengo la Timu ya Yanga si sehemu ya nyumba zitakazobomolewa katika mradi wa bonde la Mto Msimbazi.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam ameeleza kuwa nyumba zitakazobomolewa tayari wahusika walifahamishwa na wengine wamekwisha lipwa fidia, amewaondoa shaka mashabiki wa Yanga kuwa jengo la timu yao halipo kwenye orodha hiyo.

“Kufikia Februari 29 ,2024 TARURA ililipa fidia ya Sh bilioni 52.6 kwenye akaunti za wamiliki wa nyumba wapatao 2, 155 kati ya 2, 329 ambao walikuwa wameandikishwa kwenye daftari la kwanza, hivi sasa TARURA inakamilisha malipo ya fidia kwa wahusika wengine 446 waliomo kwenye daftari la pili” amesema Matinyi.

Ameongeza kuwa shughuli ya kubomoa nyumba hizo itaanza Aprili 15 mwaka huu na inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miezi mitatu hadi kukamilika kwake.

Mradi wa bonde la Mto Msimbazi unatarajiwa kugharimu Sh bilioni 675 na utakamilika ndani ya miaka mitano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live