Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jengo la Yanga kupigwa mnada

Yanga Makaoooo.jpeg Jengo la Yanga kupigwa mnada

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mara kwa  mara  jengo la Klabu ya Yanga limekuwa katika hatihati ya kutaka kupigwa mnada na Benki ya Nyumba (THB).

Ni miaka ya hivi karibuni habari za jengo hilo ndio zimepotea masikioni mwa wadau wa michezo.  Kwa hiyo sio rahisi kwa mashabiki wa soka wa miaka ya hivi karibuni kujua sababu ya jengo hilo kataka kupigwa bei.

SABABU NI UWANJA

Hivi karibuni Yanga ilimwomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani kataka kujenga uwanja wa kisasa katika sehemu ambayo zamani kulikuwa pia na Uwanja wa Kaunda uliokuwa ukimilikiwa na klabu hiyo.

Lakini  ikumbukwe mwaka 1973 Yanga ilikopa fedha katika Benki ya Nyumba kiasi cha Sh600,000 (ndio laki sita) kwa ajili ya kujenga Uwanja wa Kaunda.

Mkataba huo uliitaka Yanga kulipa deni hilo ndani ya miaka 15 kuanzia Septemba Mosi 1973 na kila mwezi ilitakiwa kulipa Sh6,500 tu.

YALIPA KIDUCHU TU

Lakini kuanzia tarehe hiyo hadi kufikia mwaka 1976 klabu hiyo ilifanikiwa kulipa kiasi cha Sh83, 000 tu, kama klabu hiyo yenye masikani yake Kariakoo katika mitaa ya Twiga na Jangwani ingetekeleza matakwa ya mkataba kisawasawa ingekuwa imeshalipa kiasi cha Sh147,000.

ILITOA HUNDI HEWA

Hata hivyo, viongozi wa Yanga kila walipokumbushwa kuhusu deni hilo wamekuwa wakiahidi kulipa na wakati mwingine wamekuwa wakitoa hundi ‘hewa’ yaani zisizokuwa na pesa katika akaunti ya klabu hiyo.

Benki ya THB ni combo cha Umma ambacho kingeweza kupata hasara kutokana na kushindwa  kulipwa malimbikizo hayo, lakini viongozi wa benki hiyo walikuwa wakitumia moyo wa ubinadamu kuisubiri Yanga kulipa deni hilo.

THB YASHANGAZWA NA YANGA

Mwaka 1976, Yanga ilianzisha mfuko maalumu wa maendeleo kutokana na pesa zilizochangwa na wanachama wake kwa lengo la kulipa madeni ya klabu hiyo.

Kitu kilichoishanga THB katika madeni yaliyohorodheshwa na klabu hiyo, deni la benki hiyo halikuwepo.

Kitendo hicho kiliwachefua viongozi wa benki hiyo na kuamua kutangaza kutaka kulipiga bei jengo la klabu hiyo lenye ghorofa tatu.

Oktoba 12, 1976 THB katika Gazeti la Uhuru likatoa tangazo ya kuliuza jengo hilo pamoja na nyumba nyingine tatu za watu wengine.

YANGA HAIKUSHTUKA

Kitu cha ajabu pamoja na taarifa hiyo, viongozi wa Yanga wakiwa na miezi tisa tangu waingie madarakani, wala hawakushtuka kutokana na tangazo hilo la benki.

MGOGORO ULICHANGIA

Uongozi wa klabu hiyo uliwatuliza wanachama na mashaki wao kwa kuwataka kutokuwa na wasiwasi.

Uongozi huo uliahidi kulipa deni hilo huku ukidai mgogoro wa muda mrefu ndani ya klabi yao ulichangia kutolipwa kwa deni hilo.

Katika mazingira ya kutatanisha, Meneja wa THB alisema wengeweza kuipa Yanga muda zaidi kulipa deni hili ili benki yake isipate hasara.

Tangu mwaka 1976 hadi miaka ya 80’ deni hilo limekuwa likitishia kuuzwa kwa jengo hilo na THB lakini hakuna kilichofanyika.

Hadi leo stori ya Benki ya THB kutaka kulipiga jengo la Yanga kutokana na deni la mwaka 1973 la kujengea Uwanja wa Kaunda (ambao haupo tena) zimebaki kuwa stori za vijiweni.  Naomba kuwasilisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live