Mchambuzi wa soka nchini Jemedari Saidi, amewataka Wana-Simba kuchangamkia tiketi za mechi ya Al Ahly kwani haiingii akili kuwepo mpaka leo hii Jumatano Oktoba 18, 2023.
Jemedari ameandika hivi;
Nyakati ambazo Mnyama anafanya yasiyotarajiwa umekaribia, Leo ni Jumatano Kesho Alhamisi halafu unaingia SIKU YA SIKUKUU YA SOKA LA AFRIKA. Simba SC wanaingia kama wawakilishi wa CAECAFA na TANZANIA kama timu iliyofanikiwa na MAARUFU ZAIDI kwenye mashindano ya CAF kutoka ukanda huu.
Nashangaa mpaka muda huu eti Wanasimba HAWAJAMALIZA kuzinunua tickets na kujipa fursa ya kuwa sehemu ya historia kubwa ya mpira wa Tanzania na Afrika.
Nimejiuliza Wanasimba nao wanataka kuwa kama TANZANIA TOURIST BOARD (TTB) ambao wametuacha kuangalia matangazo ya Visit Rwanda na kuhusiana na Utalii wa Saudi Arabia kwenye mabango ya kidijitali pale uwanja wa Mkapa Ijumaa.
Wanasimba nao wasipomaliza tickets manake waje wengine wanunue halafu wao wabaki vibanda umiza? Ili wasiwe sehemu ya historia hii kubwa barani Afrika? Watanzania huwa tunataka nini haswa, jambo hili lingefanyika kwingine tungenung’unika kuikosa fursa, leo limekuja mlangoni kwetu tuchangamkieni fursa kubwa hii. Nimeona mahala jamaa wameanza kuja kutoka nchi za jirani na zile za mbali kuja kuona Mnyama na Ahly, sasa wanasimba laleni usingizi wa pono tu.