Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari asisitiza: Goli la Azam dhidi ya Yanga haikuwa offside

Jemedari Asisitiza: Goli La Azam Dhidi Ya Yanga Haikuwa Offside.jpeg Jemedari asisitiza: Goli la Azam dhidi ya Yanga haikuwa offside

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waamuzi wetu huwa wanapuyanga sana na tunawasema tunavyotaka, basi siku kama HAWAJAPUYANGA hatuna haja ya kuwatafutia nahau, nongwa ndogo ndogo zisizokuwepo, ikibidi tuwapongeze kwa kufanya vizuri kwani nawao ni binadamu wanapenda na wanastahiki sifa njema kama wengine.

Tunapowakosea tunataka wajirekebishe wafanye vyema, wakifanya vyema tunapaswa kuwatia moyo kwa sifa ili watunze au waendeleze mambo mema.

Nasisitiza hii HAIKUWA offside na watu wanapaswa kumpongeza FRANK JOHN KOMBA kwa kuwa makini katika hili tukio, najua kama uko upande wa kupoteza inauma sana lakini ndo dawa hiyo na ili upone lazima unywe kwahiyo tuvumilie.

Kuna watu wananiandikia na kusema “oooh ilikuwa offside ya wazi, mara ilikuwa very tight” bila kutoa ushahidi wa namna gani ni offside ya wazi au very tight, hii HAIKUWA offside na Komba pamoja ni Mngoni lakini anastahiki pongezi.

Wangoni sio watu wa kuwaamini, walikimbia South Africa kuja Tanzania halafu wakaenda kuishi Songea, Namabengo, Mfaranyaki, Bombambili, etc etc, kama haitoshi wakawa wanaenda South Africa kwa Visa kabla haijaondolewa, hao ni watu kuwaamini sasa? Kama haitoshi wakajiita majina ya hovyo ya wanyama Nguruwe, Nyati, Komba etc etc. Watani zangu hawa ???? sisi Baba zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live