Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari aiponda Bodi ya Ligi timu kukaa siku nyingi bila kucheza

SAID JEMEDARI 1140x640 Jemedari aiponda Bodi ya Ligi timu kukaa siku nyingi bila kucheza

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiki mbili zilizopita vilabu vya KMC na AZAM FC vyote vya Dar es Salaam vilikubaliana kwamba wacheze mchezo wao wa Ligi kabla ya tarehe 8.12 2023 ambayo Bodi ya Ligi iliwapangia.

Hii ilitokana na ukweli kwamba kwenye ratiba za michezo yao ya mwisho vilabu hivyo vilikuwa na zaidi ya siku 15 mpaka mchezo wao huu.

Yani ratiba ya ligi yetu inatoa mwanya kwa vilabu kukaa zaidi ya siku 15 katikati ya msimu bila kucheza mchezo wa Ligi kuu, kichekesho cha karne ya 21.

Kwa sababu yoyote ile inayoweza kusemwa lakini timu kukaa zaidi ya siku 15 bila mchezo wa Ligi Kuu na zingine zinacheza na hizi timu za eneo moja hakuhitajiki hata kusafiri ni kitu cha hovyo ukitaka kuwa mkweli, mpaka vilabu vinakubaliana kurudisha mchezo nyuma kwahiyo watendaji wa Bodi wao hawaoni chochote, aisee!

Halafu kitu kingine kilipelekea vilabu kuomba kucheza mchezo huu mapema ilikuwa ni kuipa nafasi KMC ambayo ina mchezo tarehe 11.12.2023 dhidi ya Tabora United ugenini.

Kichekesho ni pale vilabu vilipokubaliana na kupeleka makubaliano yao kwa Bodi ya Ligi Kuu wiki 2 zilizopita, lakini Bodi wao wamekubali ombi hilo na kulipitisha leo tarehe 5.12. 2023 huku vilabu vikiwa vimeshapanga mipango ya mechi hiyo kuwa ni tarehe 8.12.2023.

Mtu mwingine anaweza kusema mbona ni siku 1 tu nyuma lakini ratiba ni jambo la kiufundi na linatumika kwenye kufanya maamuzi mengi ya kiufundi na kiutawala pia.

Ratiba ndiyo inayokupa uwezo wa kupanga mazoezi na mapumziko ya wachezaji mpaka siku ya mchezo husika, lakini kama unasafiri inakufanya kupanga mipango yako ya namna ya kusafiri, bookings za safari na hotel unakoenda.

Siku moja inaweza kuharibu plan nyingine nyingi mno. Bodi ya ligi haina wataalamu wa ufundi? Halafu kama mlikubali mapendekezo ya vilabu kwanini msifanye mawasiliano nao kwa haraka, kulikuwa na shida gani, hii inatoa tafsiri kwamba ofisi ina shida ya kuwasiliana na wadau wake wakubwa ambao ni vilabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live