Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said amvaa Rais Karia

Jemedari Said The Voice Less Jemedari Said amvaa Rais Karia

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka, Jemedari Said amemvaa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kufuatia maamuzi ya shirikisho hilo kupeleka mechi za Ngao ya Jamii kwenda kuchezwa katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

jemedari amesema kuwa haoni sababu ya kupeleka mechi hizo Tanga kwani ni upendeleo hasa ikizingatiwa kuwa hivi karibuni mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Azam ulipigwa uwanjani hapo.

"Karia anapeleka matukio makubwa Tanga kwa sababu yeye anatokea Tanga, hii lazima tuseme kama kuna mtu atachukia basi atajua mwenyewe, unapokuwa kiongozi wa ngazi ya juu na wewe unatokea Tanga alafu matukio makubwa kama haya unapelekea Tanga lazima watu tujue huu ni upendeleo.

"Kwanza kwa nini Tanga, wakati hata fainali ya FA uwanja haukujaa, mimi sioni sababu maalum mashindano haya kupelekwa Tanga, kwangu naona ni upendeleo, Rais analeta upendeleo mechi zote kupelekwa Tanga.

"Tanga sio kiwanja bora cha kucheza, ukitoa Kwa Mkapa basi ni Chamanzi, na mbona Kiwanja cha Chamanzi kipo tu, yeye Rais Karia anasema Tanga ni karibu, hakuna lolote huu ni upendeleo tu," amesema Jemedari Saidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: