Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said ampa za uso Manara, amshushia takwimu kumziba mdomo

JEMEDARI NA MANARA EFM Vita ya Maneno baina ya Manara na Jemedari imekuwa kubwa mno

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Nimeona clip ya KALIKONJI anazungumzia kuhusu CAF CUP ambayo SIMBA SC ikicheza fainali na Stella Abidjan na wakapoteza mabao 2-0 Dar es Salaam baada ya sare ya 0-0 ugenini."

"Anasema kombe hilo lilikuwa la Moshood Abiola wala halikuwa la CAF na kwamba nchi za kiarabu waligomea."

"Unajiuliza huyu alikuwaje kiongozi wa klabu kama Simba ambayo ina historia nzuri kwenye mpira wa Afrika? Nasema hivi kwakuwa hii ndo nafasi kubwa kwenye mpira alowahi kuishika (Afisa habari wa Simba)."

"Yanga ameingia kama Afisa Mhamasishaji akichukua nafasi ya Antonio Nugaz alipoingia Afisa habari alikuwa Hassan Bumbuli, baada ya Bumbuli ameingia Ally Kamwe."

"TUMKUMBUSHE KALIKONJI

CAF CUP ilianzishwa mwaka 1992 na aliyekuwa Rais wa CAF Issa Hayatou ambaye aliufanya mwaka 1992 kuwa mwaka wa mafanikio ya soka la Afrika, ndiyo mwaka ambao hata CAF African Cup of Nations ilikuwa na timu 12 kwa mara ya kwanza. Kombe la CAF lilipewa jina la Moshood Abiola kwa sababu za kibiashara tu, kama leo FA CUP hapa Tanzania inaitwa AZAM SPORTS FEDERATION CUP."

"Anasema timu za kiarabu baadae zilikataa hilo kombe, huu ni uwongo kwani bingwa wa mwisho alikuwa RAJA CASABLANCA ya Morocco mwaka 2003 wakicheza fainali na CottonSport."

"Kombe hilo mpaka linaunganishwa na kombe la washindi kuunda kombe la Shirikisho mwaka 2004, bingwa wake wa kihistoria ni JS Kabylie ya Algeria ambayo ilishinda mara 3, vipi JS Kabylie ya Algeria sio nchi ya Kiarabu? Simba 1993 walicheza na USM El Harrach ya Algeria."

"Kabla ya 1997 mashindano yote ya vilabu yalikuwa ya mtoano, mwaka 1998 CAF wakaanzisha Champions League na wakaweka na makundi ya timu 4 kila group ambayo Yanga walicheza."

"Wakaanzisha kuzipa timu shiriki pesa CAF walichukua hii kutoka UEFA CHAMPIONS LEAGUE. Mashindano mengi ya CAF yalianzishwa kwa kuiga UEFA."

"1974 Simba SC ndo klabu ya kwanza Tanzania kucheza nusu fainali ya vilabu barani Afrika wakicheza na GHAZL EL MEHALLA SC ya Misri..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live