Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said ainyooshea kidole TFF, acheni upendeleo

Jemedari Said The Voice Less Jemedari Said ainyooshea kidole TFF, acheni upendeleo

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Azam FC, Oktoba 23, mwamuzi msaidizi namba mbili, Kasim Mpanga, aliwanyima Azam FC nafasi hii ya bao (angalia video).

Alihukumu kwamba Dube ameotea lakini haikuwa hivyo.

Dube kwa namna ya nafasi ilivyokuwa, Dube angeweza kufunga hapa.

Kwenye mechi hiyo hiyo, mwamuzi msaidizi namba moja, Janeth Balama, aliruhusu bao la offside la Gibril Sillah.

Kwa kosa hilo, Balama akafungiwa miezi mitatu.

Hii ni double standard

Kosa la kuruhusu bao lisilo halali ni sawa tu na kosa la kukataa bao halali.

Hawa wamuzi wasaidizi wakitakiwa wote waadhibiwe.

Hii inatoa picha mbaya sana kwa mamlaka za mpira

Ukirejea matukio mengi ya miaka yote kwamba Azam FC kuwa waathirika wakubwa wa makosa ya maamuzi, unaweza kupata hisia kwamba mamlaka zinahusika.

Katika mechi moja, mwamuzi aliyeipa faida Azam FC kafungiwa. Aliyeigharimu Azam FC hajafungiwa.

Maana yake, kuigharimu Azam FC ni sawa tu, lakini siyo kuipa faida na kuipa faida Yanga ni sawa lakini sio kuigharimu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live