Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Yanga wamejitahidi

Yanga Cr Belouizdad M Jemedari Said: Yanga wamejitahidi

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga 'Wananchi' wameianza hatua ya makundi kwa kichapo cha mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Makundi baada ya kukubali kufungwa na CRBelouizdadugenini nchini Algeria.

Hii ni sawa na msimu uliopita kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho ambapo walianza mchezo wa kwanza ugenini kwa kichapo dhidi ya US MONASTIR ya Tunisia.

Mchambuzi wa Efm radio Jemedari Said Kazumari amesema;

"Sio matokeo mazuri, lakini haikuwa performance mbaya saaana, mabao yamefungwa kwenye muda ambao umakinifu huwa mdogo kitaalamu kwa wachezaji. Dakika 10 za mwanzo wa mchezo, dakika chache kabla ya mapumziko na dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho.

"Kwa muda mrefu wa mchezo Yanga wamekuwa na very impressive performance kwa wachezaji mmoja mmoja na kwa timu, bado kuna mechi 5 za kucheza nafasi ipo kubwa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live