Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Yanga imekuwa 'dampo' la Simba

Chama Ss Clatous Chota Chama

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EFM na TVE, Jemedari Said amesema kuwa Klabu ya Yanga imegeuka kuwa la Klabu ya Simba kwa kusajili wachezaji wanaoachwa na timu hiyo.

"Nimejiuliza Yanga walipanga kumtambulisha Chama kabla ya mchezaji mwingine yoyote? Uhamisho “mkubwa wa kisiasa” (Pilitical signing) unaitambulishaje, bila video, madoido na ubunifu ule ambao idara ya habari ya Yanga imezoea kuufanya na kujipatia sifa.

"Nini kimeharakisha hili kiasi Mwamba wa Lusaka kutambulishwa akiwa chumbani anasaini na kalamu ya ‘Biki’ akiwa na jacket la maskani na sio nguo rasmi za klabu? Habari zinasema Simba walikuwa wanajaribu kupindua meza kurudisha pesa za Yanga, wenzao wakawahi siku moja baada ya tarehe ya mkataba wake kuisha wakamtambulisha bila maandalizi almuradi wameshinda vita."

"SIMBA WAMEACHWA Sijapenda Simba wameachwa wakati wao walikuwa na nafasi ya kumfanyia “Send off” mtu ambaye walikuwa wanamtuhumu miaka mingi, wanaumiaje kwa mtu wa namna hii? Simba wana umizwaje na mtu ambaye wamemchoka baada ya miaka 7 ya masimango na nong’ono za kuwaumiza?"

"YANGA WAMEGEUKA DAMPO LA SIMBA? Klabu iliyofikia fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na msimu uliofuata kutinga robo fainali ya Kombe la Mabingwa wa Afrika, Mabingwa wa NBC Premier League mara 3 mfululizo na Mabingwa wa CRDB BANK Confederation Cup mara 3 mfululizo, hii ni kubwa sana na imejengwa kwa muda. Kwanini imegeuzwa sehemu ya ‘kutupia’ wachezaji wanaochoka kutoka Simba SC?

"Tuna amini Simba hawakuwa bora kuliko Yanga kwa misimu 3 mfululizo, lakini timu bora imepokea wachezaji 3 walionekana kama mzigo Simba, Austine Okra alionekana choka mbaya Simba, Yanga wakampokea, Jonas Mkude aliachwa Simba, Yanga wakambeba, Bernard Morison wakati anatoka Yanga kwenda Simba alikuwa ‘Mali safi’ ikatokea vita, siku 3 Ofisi za TFF zilifungwa kusikiliza hukumu.

"Morison alishinda vita hii CAS, Morison wakati anatoka Simba kwenda Yanga alikuwa ‘chokest’ hakua na jipya bahari ilikuwa shwari, leo Chama wakati wengi wakiamini hana jipya ndiyo Yanga wanaona anafaa," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live