Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Wanaotaja kanuni hata kanuni hawazijui

Dfb Jemedari Patrick Kocha Baraza

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amemchana Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, wakili Patrick Simon baada ya kudai kuwa kipa mpya wa Simba, Jefferson Luis hapaswi kucheza Ligi ya Tanzania kwa sababu mchezaji huyo ametoka ligi daraja dogo tofauti na kanuni za TFF zinavyotaka.

Tuliwahi kuambiwa kwamba kwa mujibu wa kanuni za CAF bingwa wetu alikuwa anaenda kuanzia first round na iwapo kama Simba, ingechukua FA Cup nao ndo wangeanzia first round.

Bingwa alibeba makombe yote akaanzia preliminary, mwaka huu kaongeza na fainali ya CAF, bado preliminary. Ndiyo maana mimi kuna wakati nikionaga watu wanataja taja kanuni huwa nakaaga kimya kabisa, najua kanuni kuzitamka kinywani rahisi sana.

Lakini kuna wakati watu wanatamka kanuni wakiwa hawazijui pengine hata hajawahi kuiona anaaumua kupiga ‘Fix’ kwa kutaja kanuni anajua watu wataona anajua sana, kumbe wapi masikini ya Mungu.

Wakati ule yanazungumzwa maoni yangu yalikuwa nani anaanzia wapi sio jambo la kila mtu kulisema kwakuwa linahitaji uelewa mpana wa mambo ya kiufundi/kimashindano, kwakuwa sio kila bingwa anaanzia first round.

Tangu Simba watambulishe kipa Mbrazil bado nasikia kanuni zinatajwa tajwa tena. Lakini ukisoma kanuni zinajieleza wazi ila kwakuwa watu ni walewale narudia tena, haya ni mambo ya kiufundi/kimashindano sio kila mmoja ana uelewa nayo wakati mwingine kuna mambo yatupite kwakuwa yatatupa aibu.

Kanauni ni jambo limekaa kisheria lakini kuna mahala pengi kwenye mashindano ya mpira linajumuisha ujuzi wa ufundi/mashindano kupata maana halisi.

Kwa mfano 1. Ligi Kuu 2. Daraja la kwanza 3. Daraja la pili 4. Daraja la tatu

Ukizihesabu namba unaona kwenye daraja la tatu kuna namba 4 ukisema kwa mujibu wa namba hilo ni daraja la 4 utakuwa uko sahihi lakini kiufundi/mashindano unakua umekosea kwakuwa hilo ni daraja la tatu tu.

Waandishi wenzangu pia tuwe makini kwenye kuripoti mambo ya kiufundi/mashindano kwakuwa yanataka utaalamu vinginevyo tutapotosha tukiona shida kutafuta wataalamu.

Nimekuja kuzika jamani bibi yangu kafa, acheni nizike nipewe mikoba tuje kupambana mjini.

NB: Mpaka sasa kama ushawahi kunikera kuna nafasi ya kuomba msamaha ukasikilizwa nikishika mkoba ni bakora tu, dereva kijana kapewa usukani sisikii la muadhini wala mnadi swala, mbweha wahed. ???????? (jokes). BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live