Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Waamuzi wanajidharaulisha, Gamondi apunguze usela

SAID JEMEDARI 1140x640 Jemedari Said

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Februari 2 2024 kwenye uwanja wa Kaitaba pale Bukoba kulikuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Yanga SC, kwenye mechi ile matokeo ya mwisho yalikuwa sare ya 0-0 ambayo kimsingi Kagera Sugar walistahili kushinda kwakuwa walikataliwa bao lao la HALALI ambalo mwamuzi msaidizi alisema mfungaji ameotea ilihali hakua ameotea (angalia video namba 2 sogeza).

Kwenye mechi ile iliyotawaliwa na maamuzi mengi ya hovyo kutoka kwa waamuzi hakukuwa na mchezaji wala mtu wa benchi la ufundi aliyemzonga na kumsukuma mwamuzi yoyote wakati na baada ya mchezo.

Kamati ya uendeshaji wa ligi ndiyo iliwahukumu, huu ndiyo weledi kutoka kwa wachezaji na benchi la Kagera Sugar, Gamondi anapaswa kujifunza huku. Siku ile yeye pale Kaitaba aliona raha Kagera Sugar wanadhulumiwa, jana analeta usela wa Tandika. Kweli mkuki kwa Nguruwe kwa Binadamu mchungu.

Nchi haina tena waamuzi wenye kuyajua mamlaka yao kiwanjani na kuyatumia ipasavyo bila kumpunja yoyote kwa kumuonea au kumpendelea.

Angalia video ya kwanza eti mwamuzi anapitia misukosuko yote hiyo halafu anashindwa walau kutoa kadi ya njano tu! Anajigeuza msuluhishi wa kimataifa anambembeleza Gamondi ambaye anafanya ushamba usio na mpango.

Lakini mwamuzi huyu alikuwa wa kwanza kuwaonyesha kadi za njano madaktari wa Kagera Sugar walioingia kiwanjani kujaribu kuokoa uhai wa mchezaji wao kama taratibu zinavyotaka bila kujali wameruhusiwa au laa. Nani alijua namna gani mchezaji yule ameumia? Madaktari wangeacha afe mbele yao? Mwamuzi akakurupuka na kadi ya njano mithili ya mtu anaona watu wanamharibia jambo lake analotamani litokee.

Mwamuzi wa mwisho nchi hii kuwa na mamlaka na kuyatumia ipasavyo alikuwa Israel Mujuni Nkongo tu, pamoja na mapungufu yake mengine kibinadamu, lakini ujinga ule lazima angekuadhibu tu. Ajabu Mujuni ni mkufunzi anazalisha hawa waamuzi na ni mkufunzi wa FIFA, nitamtafuta nimuulize huwa anawafunza nini hawa watu. Haya ndo mafunzo yenyewe? Waamuzi wanajidhalilisha sana kwa kushindwa kuchukua hatua maeneo ya wazi kama haya, hawatokaa waheshimike miaka na mikaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: