Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Tutangulize Maslahi ya Soka si vinginevyo

Karia X Jemedari Said Jemedari Said: Tutangulize Maslahi ya Soka si vinginevyo

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wameiomba Bodi ya Ligi Kuu mchezo wake wa raundi ya 3 dhidi ya Coastal Union uchezwe mapema kabla hawajaingia kwenye mashindano ya kimataifa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, zimebaki kama siku 20 waingie huko.

Simba wanadhani mchezo dhidi ya Coastal Union ambao kwenye ratiba unaonyesha TBA (To be arranged/announced) kwenye tarehe ikiwa na maana itatangazea baadae, uchezwe mapema kupunguza viporo kwakuwa wao wana hizo siku 20, Coastal pia wana siku sio chini ya 14 bila mechi.

Majibu ya Bodi ni kwamba mchezo huo hauwezi kuchezwa kwakuwa Coastal Union wamewaruhusu wachezaji wao kupumzika na watarudi kambini Alhamis. Ajabu ilioje, baada ya mechi 2 timu zina zaidi ya siku 14 kupumzika, Simba wanatamani mpira uchezwe Bodi wanataka timu zipumzike na Coastal wamerejesha wachezaji majumbani.

Mwaka huu Simba wanacheza African Super League, kuanzia Oktoba 20 mpaka Novemba 20 Simba hawtocheza mechi za nyumbani, michezo yao itasimama. Wakiingia nusu fainali watapata siku 10 zaidi bila michezo ya nyumbani.

Wanafikiria kupunguza viporo ligi isipungue ladha sana huko baadae, wenzetu wanaifikiria Coastal wakicheza na Simba wakati huu wanaweza wakapigwa nyingi, kuwaokoa ni kuikataa mechi mpaka hapo baadae waipachike popote pale.

Coastal wako tayari kucheza mchezo wa raundi ya 4 kabla ya huu wa raundi ya 3 ambayo ni kituko kwakuwa raundi ya 4 wanacheza na KITAYOSCE

Coastal Union Mwenyekiti wake ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, mwanachama wake mkubwa ni Rais wa TFF kaka yangu Wallace Karia, kwahiyo kuna wakati wanaelea kwenye mapenzi mazito kwakuwa wao ni “Last Born” wa TFF.

Msimu uliopita walibadilishiwa ratiba yao dhidi ya Geita bila maelezo kwakuwa tu walikuwa wanakaa Mwanza wiki nzima kabla ya mchezo na Geita, Bodi wakalazimika kubadili ratiba Last Born acheze mapema kisha arejee Tanga.

Bodi wajiangalie na kuangalia maslahi ya soka sio nasaba ya viongozi na vilabu. Kama wako makini mchezo wa Simba Coastal uchezwe kabla Simba hawajaenda kimataifa vinginevyo huu upendeleo kwa Coastal utakuja kuwatafuna huko mbele na unawachafua Karia na Mnguto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live