Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Simba akishinda fresh, Yanga amenunua mechi?

SAID JEMEDARI 1140x640 Jemesari Said

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa Soka nchini, Jemedari Said amewashtukia baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakiponda ushindi wa Klabu ya Yanga wakidai kuwa ananunua mechi pasi na uthibitisho wa kauli hizo.

Kauli hiyo ya Jemedari inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Yanga kuichakaza vibaya Singida Big Stars hapo jana kwa kuifunga bao 4-1 katika Dimba la Mkapa.

"Hii Nchi ina watu wa ajabu sana, Yanga ambao ni mabingwa wa vikombe vyote vya ndani kushinda (4-1) dhidi ya Singida eti wamenunua mechi,, Simba kushinda (5-0) dhidi ya Mtibwa tena yenye Wachezaji (9) kimyaa hakuna aliyesema Simba wamenunua mechi.

"Kuna watu wa hovyo sana nchi hii. Golikipa wa Singida Khomein alikuwa na mapungufu ndio lakini alifanya mapungufu makubwa zaidi kwenye mchezo dhidi ya Simba yakasababisha Peter Banda akamfunga kizembe kabisa lakini hakuna aliyesema Simba kanunua mechi.

"Huu ni ujinga haupaswi kuachwa hivihivi bila kukemewa,, Kwa hiyo Yanga hii haina uwezo wa kumfunga Singida ?.. Ni ujinga tu," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live