Mchambuzi nguli wa Masuala ya soka nchini Tanzania, Jemedari Said Kazumari kupitia kipindi cha Sports HQ cha EFM amesema Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' anajidanganya kulinganisha kikosi chake na wapinzania wao Raja Casablanka.
Kauli hiyo ya Jemedari inakuja baada ya Robertinho kusema kuwa wanafahamu Raja ni timu kubwa Afrika lakini pia SImba ni timu kubwa vile vile.
"Kocha Mkuu wa Simba, Robertinho anasema anajua Raja Casablanca ni timu kubwa Afrika lakini Simba pia ni kubwa Africa hivyo anaweza kushindana nayo.
"Zama za kutudanganya zimeshapitwa na wakati, huwezi kuiweka Simba daraja sawa na Raja Casablanca ni vyema akajipanga vizuri katika mchezo ujao.
"Kwenye ukanda wa CECAFA Timu pekee inayoweza kuwekwa mizani sawa na vilabu vya Kaskazini ni Al Hilal pekee," Mchambuzi Nguli Jemedari Said Kazumari Kupitia Sports HQ ya EFM.
Ikumbukwe kuwa, baada ya kipigo cha bao 1-0 wakiwa ugenini nchini Guinea dhidi ya Horoya, Kikosi cha Simba kitaingia Dimbani Februari 18, 2023 katika dimba la Mkapa kuvaana na Raja Casablanca katika mchezo wa mzunguko wa pili wa kundi C wa Kombe la Mabingwa Afrika.
Raja tayari wana alama tatu kibindoni baada ya kuifunga bao 5-0 Vipers United ya Uganda huku Horoya nao wakiwa na alama 3 baada ya kuifunga Simba bao 1-0.