Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Gamondi alikuwa sahihi kubadili kikosi dhidi ya Ihefu

SAID JEMEDARI 1140x640 Jemedar Said

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga Jana walipoteza mchezo wao wa kwanza wa Ligi msimu huu dhidi ya Ihefu Jijini Mbeya katika Uwanja wa Highland Estates.

Yanga ilikubali kipigo cha Mabao 2-1, lakini kikosi kilichoanza katika mchezo huo kilikuwa na mabadiliko makubwa.

Wengi wameonekana kumlaumu Kocha kwa kitendo cha kuwaacha nje wachezaji 8 wa kikosi cha kwanza.

Sasa Mchambuzi wa Michezo kutoka Efm, Jemedari Said amemkingia kifua Kocha huyo na kudai kuwa alikuwa sahihi.

Akizungumza Jemedari anasema;

"Kama huu ulikuwa wakati mzuri wa kufanya mabadiliko ya kikosi cha kwanza cha Yanga, binafsi yangu ninaamini ilikuwa nafasi nzuri ya kufanya mabadiliko ya kikosi. Ukiichukua Yanga ukiilinganisha na Ihefu, bila shaka utasema Yanga ni kubwa sana kwa Ihefu."

"Kama Yanga wangefanya mabadiliko dhidi ya zile timu kubwa nne kwenye ligi kuu basi yangekuwa makosa lakini kufanya mabadiliko kwenye mechi dhidi ya Ihefu binafsi yangu naamini ulikuwa wakati sahihi haswa kwa kuwa timu imetoka kwenye michuano mikubwa."

"Kama mwalimu ni jukumu lake kuhakikisha kila mchezaji anafuraha lakini pia kila mchezaji anaongezeka kiwango lakini pia una mechi tarehe 4 na una mechi tarehe 7, kwanini usifanye mabadiliko ya kikosi?"

Je, unakubaliana na Jemedari Said? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: