Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Bacca Day ni siku ya Yanga kufuta ujinga

Jemedari X Bacca Day Jemedari Said: Bacca Day ni siku ya Yanga kufuta ujinga

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama Gongowazi wanataka kukanusha ujinga wa kwamba wenye akili kwenye timu ni 2 tu, basi siku ya kufanya hivyo ni tarehe 02-12-2023 pale Kwa-Mkapa.

Kutokana na umuhimu wa mechi hii sioni namna gani GONGOWAZI kindakindaki anawezaje kubaki nyumbani kuliko kwenda Taifa kujaza kiwanja na kuwapa sapoti wachezaji. Hii ndiyo mechi itakayowapeleka ROBO FAINALI kama wana macho ya kuona kilichojificha.

Alama 3 au 1 kwenye mechi hii ndo inaweza kuwavusha baaden, lakini kupata hiyo 1 au zote 3 sio rahisi kama wanavyodhani na kujidanganya eti Ahly WACHOVU siku hizi. WACHOVU kwa kuangalia wanapigana na wengine ni kujiambia uongo mchana kweupe.

Vaeni misuli au vikoyi na jezi zenu, ndani msivae chochote yani muwe WAZI (Chukuchuku au Chiyembeyembe) kama mnavyoambizani lakini kwa heshima kubwa sana. Mnapaswa kujaza kiwanja kutengeneza mazingira ya ugeni kwa Ahly na mjitolee kushangilia kuwapa nguvu wachezaji.

Mkienda mnasema mnacheza na WACHOVU huku baada ya msuli au kikoi hakuna kizuizi, mtatupa connection nyingine kuliko za Gift.

Ushindi unaweza kupatikana na mmoja wa wanoutamani sana lakini natoa tahadhari kwa namna watu au Gongowazi wanavyojionyesha kwamba wanakwenda kuokota tu na kuondoka, Hapana, wale Ahly Mabingwa watetezi na Mabingwa wa kihistoria wa CAFCL.

Nataka muwe watupu ndani halafu muwe kiwanjani kama Ally Kamwe @alikamwe anavofanya kazi njema kuwahamasisha, mshike HASHUA zenu mzibinye kwa maana ya kubinya ikiwa kama ni dawa ili ushindi upatikane. SÄ°LAHA YENU YA KWANZA MKAJAZE KWA-MKAPA na hii ndiyo kitu pekee ambacho hakika mnaweza, vingine vibaki kwa Garmondi na vijana wake nyinyi mshike hashua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live