Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Azam FC wasichukuliwe poa, wana timu na vilevile wamejipanga

Jemedari X Azam FC Jemedari Said: Azam FC wasichukuliwe poa, wana timu na vilevile wamejipanga

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimesoma mahala Afisa habari wa Azam FC Hasheem Ibwe amenukuliwa akisema “tukianza kudekezwa kama wao tutachukua kikombe mara 10 mfululizo”, ukiangalia kwa juu juu kauli ya Ibwe na kimazoea utaibeza na kumuona hana lolote. Lakini ukweli ni kwamba mfumo wa mpira wa nchi unazibeba Simba na Yanga kwa kiasi kikubwa, kama hujui hili utakua uko mbali na mifumo ya mpira wa nchi na sikulaumu.

Azam FC ndiyo klabu pekee msimu huu imeanza kufanya usajili ambao unaonekana wameufanyia scouting, ndiyo wachezaji wanaweza kuchukua muda kuzoea ligi na maisha ya bongo wakachelewa kuwapa wanachotaka lakini hamna shaka sana kwakuwa usajili ni kamari, ikitokea wakaingia kwenye mfumo wakatoa walichokiona viongozi na kikaleta manufaa basi watakuwa hatari sana msimu ujao.

Si mbaya sana kama mifumo ya ndani kwa sababu ambazo hata wao wanazijua ikiwakataza kupata ubingwa, lakini kuna ishara ya huenda wakapata kucheza group stage ya vilabu barani Afrika kwa mara ya kwanza tangu klabu kuundwa. Nafikiri hiyo itafikisha kwa kiasi kikubwa meseji ya Ibwe kwa wahusika.

Tangu ligi inaelekea kuisha na mpaka wanafunga msimu Jumapili, Azam FC walikuwa wanajua wanamsajili nani na kwa şababu gani, hivyo ndivyo modern football club inavyopaswa kuendeshwa. Unafanya scouting ligi zinaendelea mnafanya mazungumzo na wachezaji na vilabu vyao kama wana mikataba mwisho mnasajili na kutangaza.

Sipati picha kama sajili hizi za Azam FC zingekuwa zinafanyika Kariakoo na wachezaji wanatangazwa manane ya usiku kama tunakula daku ingekuaje, au adhuhuri baada ya swala kama tungeishi mjini, tungeambiwa D’salaam umeme utazimika wiki 3. Azam FC wanafukuza mwizi kimya kimya kama Jay Moe @jaymoefamous Mmachinga mwenzangu na nchi imetulia.

Azam FC wana wachezaji 6 kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoenda Malaysia na wana Sospeter Bajana aliye majeruhi kufanya idadi ya wachezaji 7 kwenye timu ya nchi. Hii ni idadi ambayo ukichanganya na wageni wanakupa mchanganyiko wa kugombea kikombe cha nchi na kucheza group stage ya shindano lolote la Afrika. Hata Simba na Yanga wanakuaga wametawala hivi Taifa Stars ili kusumbua ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live