Picha ya juu ilipigwa tarehe 6. Juni. 2023 Chamazi Complex, ilikuwa baada ya mchezo Simba SC na Polisi Tanzania.
Matokeo yalikuwa ushindi wa bao 6-1 kwa Simba na Saido Ntibazonkiza alifunga mabao 5 peke yake. Kwahiyo hapo alikuwa anakabidhiwa mpira wa mechi na mwamuzi wa mchezo huo kutoka Tanga ndugu Omari Mdoe.
Picha ya chini imepigwa tarehe 21. Septemba, 2023 uwanja wa Uhuru kabla ya mchezo kati ya Simba na Coastal Union ya Tanga.
Matokeo Simba SC walishinda 3-0 mabao yote alifungiwa Jean Baleke, lakini katika picha anaonekana Saido anapewa mpira na Daud Kanuti moja ya viongozi wasimamizi wa mechi.
KILICHOJIRI
Baada ya Saido kufunga mabao 5 tarehe 6 Juni na kupiga picha kama anapewa mpira na mwamuzi Mdoe kumbe zilikuwa ‘Fix’ tu jamaa waliondoka na mpira wao na Saido aliondoka mikono mitupu.
Sasa jana ndo kabla ya mechi akawa analipwa ule mpira wake ambao alipokonywa baada ya kukabidhiwa tarehe 6 Juni, yani miezi 3 na siku 15 baadae..!!!
Kulikuwa na ulazima gani wa kumkabidhi mpira Saido mbele ya Camera na kupiga picha kujitia aibu na kuwatafuta watu maneno tu. Kwanini baada ya kumpokonya pale Chamazi bila Camera, wasingemfuata kambini wakamkabidhi bila Camera kama alivyompokonya? Aibu hii inaepukika ndugu zangu mmejitakia tu. Sasa tunajiuliza wangapi wanatunukiwa na kupokonywa tunu zao na hatujui?