Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jembe: Nilijua tu Benchikha ataondoka Simba

Benchikha Simba 29 At 22.jpeg Abdelhak Benchikha.

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally 'jembe' amesema kuwa alijua kuwa Kocha Abdelhak Benchikha angeondoka ndani ya Klabu ya Simba kutokana na kushindwa kupata matokeo mazuri tangu ametua kwenye timu hiyo.

Jembe amesema hayo baada ya Benchikha kubwaga manyanga na kusepa kwao nchini Algeria kwa madai kuwa anakwenda kumuuguza mkewe.

“Mimi nilikuwa naiona dalili, kwa hali ilivyokuwa inakwenda Simba alikuwa hana ujanja. Kaitoa Simba kwenye Champions League hatua ya robo fainali, hatua ambayo Simba tayari walikuwa nayo misimu kadhaa nyuma.

“Amefungwa na Al Ahly nyumbani na ugenini jambo ambalo halijawahi kutokea kwa Simba. Michuano ya Kombe la Shirikisho wametolewa na timu iliyoshuka daraja tena ikiwa pungufu baada ya kupewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.

“Watanzania watasema kocha hana tatizo, tunatakiwa tujue kocha anapimwa kwa matokeo wala si kwa muonekano wake, sura, upole, kipara chake au kofia yake, ni takwimu ndizo zinampima kocha. Washambuliaji wake hawafungi, mabeki wanafungisha, hili ni jukumu la kocha. Tumeambiwa ameondoka kwa sababu ya jambo la mkewe, tunapaswa kuliheshimu, nimeambiwa ni mgonjwa wa kansa, Simba wameonesha uungwana.

“Kitakwimu Benchikha alipaswa aondoke aidha kwa yeye mwenyewe kuomba au Simba kumuondoa. Sasa hivi kuna tatizo la kocha, uongozi na tatizo la kikosi, niliona ataondoka na hasa baada ya kupoteza kombe la shirikisho kwa sababu pengine Klabu Bingwa ilikuwa mfupa mgumu kwao. Wangepambana na Shirikisho na Ubingwa. Simba angetolewa na Azam au Yanga ungesema ukubwa wa hizi timu umechangia lakini Mashujaa? Lazima Benchikha angeondoka tu.

“Kusema tatizo ni wachezaji na sio benchikha mimi nakataa, wangepata Ubingwa kocha angepewa sifa, kwa nini ikishindwa tatizo liwe wachezaji yeye ameshindwa vipi kuwabadilisha wachezaji wake? Timu ya mpira ikikosa matokeo inashuka ubora na kushuka thamani yake, Simba wanapaswa wawe makini sana na hilo,” amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live