Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je, Messi alistahili kutwaa Ballon d’Or?

Gettyimages 1236893307 Lionel Messi Wins 2021 Ballon D Or 1400 Mshindi mara saba wa tuzo ya Ballon D'or

Tue, 30 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana usiku, nyota wa PSG na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or. Hii ni mara ya 7 kwake, alistahili?

Tuzo za Ballon d’Or ni miongoni mwa tuzo kubwa kwenye ulimwengu wa soka. Ni mbio na ushindani mkubwa kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao kwa sasa, Leo anaongoza kwa tuzo 2 zaidi ya CR7 (tuzo 5).

Kwa wengi, mpaka leo, haijulikani ni vigezo vipi hasa vinatumika kumpata mshindi wa tuzo hizi. Kama ni viwango uwanjani, kwa msimu husika? Tuzo zipo kibiashara zaidi? au sababu nyingine yeyote mbali na kura zinazopigwa na makocha, manahodha wa vilabu na mamlaka zingine zinazohusika.



Pamoja na kupokea pongezi za kutwaa tuzo, kuna hali ya sintofahamu kama kweli Messi alistahili tuzo hiyo. Sintofahamu hii inakuja kutokana na ubora walioonesha wachezaji wengine waliokua kwenye kinyang’anyiro hicho.

Robert Lewandowski (Bayern Munich na Poland), amekuwa kwenye kiwango bora kwa misimu takribani minne mfulululizo. Takwimu zake za kutwaa mataji na kubeba tuzo mbalimbali ni kubwa kulinganishwa na Messi kwa misimu mitatu mfululizo (2019/2020,2020/21 na 2021/22) lakini, Lewandowski hajapewa tuzo ya dunia.



Kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya Italia, Jorginho, alikuwa kwenye kiwango thabiti msimu uliopita (2020/21). Alitwaa Ubingwa wa UEFA, Super Cup na EURO 2020 lakini, yeye pia hajafua dafu ya Leo ambaye, alimaliza msimu uliopita kwa kutwaa taji la Copa America na Copa del Rey pekee akiwa amepachika magoli 38 kwenye mashindano yote aliyocheza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live