Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Je, Ligi ya Bongo ni ngumu?

Elvis Rupia Vs Mtibwa.jpeg Je, Ligi ya Bongo ni ngumu?

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu 2022/23 Elvis Rupia aliibuka mfungaji bora kunako ligi kuu ya Kenya [FKFPL] akiwa na klabu ya Police Kenya,Alifunga mabao 27 akimpiku Benson Ochieng Omalla wa Gor mahia ambaye alifunga 26.

Msimu 2023/24 makachero wa Singida Fountain gates walimng'oa Rupia kule Police na wakamleta kwenye jumba la ladha na heka heka,

Usajili wa Rupia ulilenga Kuongeza nguvu kwa Thomas Ulimwengu,Habibu Kyombo,Fancy Kazadi ambao walikuwa na Singida Fountain gates.

Rupia akiwa na Singida Fountain gates na baadae Ihefu Sc ambayo anaitumikia mpaka sasa kwa pamoja amecheza michezo 17 na kufanikiwa kufunga mabao 4 tu huku ikiwa imesalia michezo michache ligi kumalizika.

Elvis hajafikia hata nusu ya kasi ya upachikaji wa mabao ambayo alionyesha pale Police Kenya msimu uliopita.Matqrqjio yamekuwa tofauti kidogo kwa waliomuona kuja kupambana kwenye jumba la ladha na hekaheka za Ligi Kuu

Je, kwa haya ya Rupia ni kipimo kuwa ligi kuu ya Tanzania ni ngumu au kiwango cha mchezaji kimeshuka kiasi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live