Rais mpya wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, Bola Tinubu, amemteua mchezaji wa zamani wa timu ya taifa hilo, Augustine Azuka Okocha almaarufu Jay Jay Okocha, 46, ameteuliwa kuwa Waziri wa Michezo, Vijana na Maendeleo.
Okocha alicheza Eintracht Frankfurt, Fenerbahçe, Paris Saint Germain (PSG), na Bolton, na timu ya taifa alicheza kati ya miaka ya 1993 na 2006 ni bingwa wa Olimpiki mwaka wa 1996, mshindi wa CAN 1994, 2000.
Okoch ambaye ana mabao 14 katika michezo 73 ya timu ya Taifa, alipigiwa kura mchezaji bora wa CAN 2004.
Jay Jay Okocha alijulikana uwanjani kwa kupiga chenga zake za kutatanisha na upigaji wa mipira iliyokufa sasa ni waziri.