Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jay Jay Okocha afafanua jina lake la utani

Jay Jay Okocha Afafanua Jina Lake La Utani Jay Jay Okocha afafanua jina lake la utani

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuhusu asili ya jina lake la utani, Jay-Jay, ambalo wengi hudhani lilitokana na kuwa alikuwa yuko vizuri sana katika uchezaji wa mpira wa miguu na hivyo kupewa hilo, yeye amesema kwamba jina hilo lilitokana na jina la kaka yake.

"Jay-Jay ndilo lililopo kwenye pasipoti yangu sasa, lakini awali, lilikuwa jina la kaka yangu mkubwa. Yeye pia alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu. Lakini labda nililipeleka jina hilo kwenye kiwango kingine," amesema Okocha

Aliweka wazi kuwa jina la kaka yake lilikuwa James Junior; “Kwa hivyo ili kunitambulisha kama ndugu yake, walinipa jina Augustine Jay-Jay. Baadaye, ilikuwa rahisi zaidi kuniita Jay-Jay kuliko Augustine Azuka. Kwa hivyo, nilichukua jina hilo," amefichua katika mahojiano na Mwananchi Digital.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live