Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jap Stam: Mikel Arteta ana mtihani mzito

IMG 4628.png Jap Stam: Mikel Arteta ana mtihani mzito

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Uwezo wa Jurrien Timber wa kucheza kama Mlinzi wa Kulia ama wa Kati, umetabiriwa kuwa mtihani mkubwa kwa Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta juu ya namna ya kumtumia mchezaji huyo.

Timber anatarajiwa kutangazwa kuwa mchezaji wa Arsenal wakati wowote juma hili, kufuatia taratibu zake za uhamisho kutoka Ajax Amsterdam ya Uholanzi kuwa kwenye hatua za mwisho.

Aliyemtabiria Arteta kuwa na kazi kubwa katika matumizi ya Beki huyo ni Kocha Mkuu wa Ajax Amsterdam Jaap Stam, ambapo amesema amesema: mchezaji huyo wa kucheza namba nyingi, akisema: “Unapokuwa mchezaji wa Kidachi na umekulia kwenye akademia, basi watu wanatarajia mengi kutoka kwake, hata kama ni beki, linapokuja suala la kutembea na mpira. Ana kasi sana. Anaweza kucheza beki ya kati na beki ya kulia, kwa kifupi ni kiraka.”

Ni mmoja kati ya mabeki wa kati watatu waliotumika kwenye kikosi cha Oranje na Kocha Louis van Gaal huko Qatar, ambapo Denzel Dumfries alitumika kwenye wing-back ya kulia.

Stam ambaye ni Beki wa zamani wa Manchester United, alimuona Timber kwenye kikosi cha vijana cha Ajax, amezungumzia uzuri wa Beki huyo anaweza kushambulia kwa ubora mkubwa kama ambavyo Oleksandr Zinchenko amekuwa akifanya, hivyo Arteta atakuwa na watu hatari kwenye pande zote mbili, kulia na kushoto.

Timber ni moja kati ya mastaa watatu wa kiwango bora kabisa kwenye kikosi cha Arsenal waliotumia katika dirisha hili na wengine ni Kai Havertz na Declan Rice.

Kwa maelezo hayo ya Stam, bado haifahamiki Timber atakwenda kutumika kwenye nafasi gani katika kikosi cha Arsenal. Beki wa kulia yupo, Ben White ambaye atashindania namba.

Usajili wa Timber unatajwa kuigharimu Arsenal Pauni 40 milioni pamoja na nyongeza nyingine ambayo inafanywa siri.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amecheza mechi zaidi ya 100 kwenye kikosi cha Ajax na aliitumikia Uholanzi kwenye Euro 2020 na Kombe la Dunia 2022.

Chanzo: Dar24