Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamie Carragher: Salah ataondoka tu

Carragher X Salah Jamie Carragher: Salah ataondoka tu

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Liverpool, Jamie Carragher anaamini Mohamed Salah ataondoka katika klabu hiyo siku za usoni baada ya dili kubuma katika dirisha la usajili la kiangazi.

Mchambuzi huyo wa Kituo cha Televisheni cha Sky Sports alitoa maoni yake akidai ni suala la muda tu na hatashangaa kama Salah akiondoka katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

“Mkataba wake utamalizika kabla ya mashabiki kujua. Nadhani hisia za mashabiki wengi wa Liverpool wanadhani Salah atacheza zaidi ya msimu mmoja.

Kama Liverpool itamuuza Salah itapata pesa ndefu na itasajili mbadala wake siku za usoni, lakini ngumu sana kupata mchezaji wa ubora wake, labda atatokea sijui nafikiri. Liverpool ina miezi 12 ya kufikiria mchezaji mwingine ambaye atakuja kuziba pengo lake.”

Taarifa ziliripoti Salah alilazimisha kuondoka Anfield hata hivyo, Liverpool ilisisitiza nyota huyo wa kimataifa Misri hauzwi kwa dau lolote.

Al-Ittihad ilikuwa na nia ya dhati ya kumsajili Salah na ilitoa ofa zaidi ya Pauni 200 milioni hata hivyo Liverpool ikapiga chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live