Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jamhuri sio wepesi, tutapambana - Matola

Matola X Miquissone Jamhuri sio wepesi, tutapambana - Matola

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku.

Matola amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao wanategemea utakuwa mgumu.

Matola ameongeza kuwa Jamhuri haikufika hatua hiyo kwa kubahatisha bali imepambana kwahiyo haiwezi kuwa mechi rahisi leo.

“Haitakuwa mechi rahisi, Jamhuri ni timu bora na haikufika hatua hii kwa bahati mbaya imepambana, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejipanga.”

“Kwa upande wetu tumejiandaa vizuri, wachezaji wapo kwenye hali nzuri lengo letu ni kuhakikisha tunashinda na kuingia nusu fainali,” amesema Matola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live