Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Jambo kubwa ni kuisaidia timu kwanza-Bocco

2K2A8211 Scaled (1) Nahodha wa Simba, John Bocco.

Wed, 23 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ kwenye ushindi 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana, Nahodha John Bocco amesema kitu cha kwanza ni kuisaidia timu kupata ushindi mengine yanafuata.

Bocco amesema kufunga mabao matatu ni jambo zuri lakini yeye anaangalia zaidi kuisaidia timu kupata ushindi na kuwapa furaha mashabiki.

Nahodha Bocco amesema lengo ni kuhakikisha anatumia vizuri kila nafasi anayoipata uwanjani ili kuifanya timu kupata ushindi.

“Jambo la kwanza ni kuisaidia timu kupata ushindi halafu mengine yanakuja kama ziada. Kufunga hat trick ni jambo jema ila timu kwanza,” amesema Bocco.

Kwa muda mrefu Bocco amekuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha na juzi  ndiyo amerejea na kufunga hat trick.

Chanzo: Eatv