Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jahmuri Dodoma yapigwa pini

Jahmuri Dodoma Yapigwa Pini Jahmuri Dodoma yapigwa pini

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeuondoa uwanja wa Jamhuri uliopo jijini Dodoma katika orodha ya viwanja vinavyotumika kwa michezo ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025, baada ya kupoteza sifa zilizoainishwa kwenye kanuni na sheria za mpira wa miguu.

Taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo imesema kuwa Eneo la kuchezea (pitch) la uwanja wa Jamhuri limeonekana kukosa ubora ambapo sehemu kubwa haina majani ya kutosha na yaliyopo ni dhaifu jambo linaloufanya uwanja huo kutokuwa salama kwa wachezaji.

Kufuatia uamuzi huo, klabu ya Dodoma Jiji sasa italazimika kutafuta uwanja mwingine miongoni mwa viwanja vilivyopitishwa kutumika kwa michezo ya Ligi kuu kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani hadi pale uwanja wa Jamhuri utakapokuwa umefanyiwa maboresho ya kuondoa mapungufu yaliyoainishwa.

Katika taarifa hiyo pia Bodi ya Ligi imezikumbusha klabu zote kuhakikisha zinaendelea kutunza miundombinu ya viwanja vyao katika kipindi chote cha msimu wa Ligi kwani kushindwa kufanya hivyo kutashusha ubora wa viwanja vyao na kusababisha viondolewe kwenye orodha ya viwanja vinavyotumika kwa michezo ya Ligi.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kuanza kwa msimu huu bodi hiyo na shirikisho la soka nchini TFF waliahidi kuwa wakali juu ya uzingatiaji wa sheria namba moja ya mpira wa miguu inayohusu miundombinu ya viwanja vya michezo huo pendwa duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: