Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jackson awashangaa mabosi Chelsea

Nicholas Jackson Chelseaaa STRAIKA wa Chelsea, Nicolas Jackson

Wed, 22 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

STRAIKA wa Chelsea, Nicolas Jackson ameweka wazi hisia zake baada ya mabosi wa The Blues kuthibitisha Kocha Mauricio Pochettino anaachana na timu hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham, Pochettino alichukua mikoba ya kuinoa Chelsea kwenye majira ya kiangazi mwaka jana, akiongoza timu hiyo kumaliza kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu. Chelsea imepoteza mechi moja tu kati ya 15 za mwisho ilizocheza kwenye ligi na mechi hiyo moja ni ile waliyopambana na Arsenal.

Chelsea imemaliza pointi tano nyuma ya kuifikia Top Four inayotoa tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Jackson amekuwa na wakati mzuri chini ya Pochettino, aliguswa sana kwa tukio hilo la Pochettino kufunguliwa mlango wa kutokea huko Stamford Bridge.

Staa huyo aliamua kwenda kuonyesha hisia zake kwa kuposti kitu huko Instagram, alipoweka emoji mbili za mikono ikiziba uso na kuandika "Nakupenda kocha."

Straika huyo Msenegali aliongeza: "Natamani tungeendelea kuwa pamoja kwa muda zaidi. Mungu azidi kukubariki wewe na familia yako. Nashukuru kwa ushauri na sapoti, wewe ni mpambanaji, kila la heri."

Jackson aliposti pia kwenye Instagram picha yake na Pochettino ya Novemba mwaka jana na matokeo ya mechi za ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Spurs na ile ya sare ya 4-4 na Manchester City na katika mechi hizo, Jackson alifunga mabao manne.

Chanzo: Mwanaspoti