Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jackson akusanya viatu klabuni kupeleka kwao Senegal

Jackson Viatu Jackson akusanya viatu klabuni kupeleka kwao Senegal

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika Nicolas Jackson huenda ameonyeshwa kadi nyingi za njano zinazolingana na mabao aliyofunga kwenye Ligi Kuu England na kuona kwamba pengine mchezaji huyo ni katili sana.

Lakini, unaambiwa hivi, straika huyo wa Chelsea, ana moyo wenye huruma na kujali wengine kuliko unavyodhani. Kwenye makuzi yake, staa huyo wa Senegalhakuwahi kumiliki viatu vya kuchezea soka hadi alipotimiza miaka 16, wakati anakua huko Ziguinchor.

Kitu hicho kinamfanya Jackson asisahau licha ya sasa kuwa na maisha mazuri na anachofanya kipindi hiki ni kusaidia watoto wa kijiji kwao. Wakati anakipiga Villarreal na Mirandes za huko Hispania, Jackson alikuwa akikusanya viatu vya wachezaji wenzake ambavyo walikuwa hawavivai tena baada ya msimu kumalizika na kuvipeleka kwao, sambamba na jezi, soksi na vikinga ugoko ili kuhakikisha ndoto za vijana wa kwao wanaotaka kucheza mpira, hazifi.

Kila mwisho wa msimu alikuwa akikusanya vitu kwenye maboksi na kugharimia usafiri — licha ya kwamba hata kipindi hicho hakuwa akilipwa pesa nyingi kwenye timu alizokuwa akichezea, huku gharama za mizigo kwenye ndege ilikuwa mara tatu ya bei ya tiketi.

Kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Chelsea, baada ya kuanza vibaya siku za hivi karibuni, straika huyo ameanza kujipata. Jackson ameonyeshwa kadi tano za njano, lakini amekuwa na kiwango kinachoridhisha akifunga mabao tisa, bao moja tu pungufu ya aliyofunga Didier Drogba msimu wake wa kwanza Stamford Bridge.

Chanzo: Mwanaspoti