Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jack Wilshere aitwa Marekani

Jack Wilshere (17).jpeg Jack Wilshere aitwa Marekani

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Colorado Rapids imefanya mahojiano na Kocha wa Timu ya vijana ya Arsenal na kiungo wa zamani, Jack Wilshere kuhusu nafasi iliyo wazi ya kocha mkuu wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS), kwa mujibu wa ESPN.

Rapids inamilikiwa na Kroenke Sports & Entertainment, ambao pia wanaimiliki Arsenal, na sasa inafanya mazungumzo na Wilshere mwenye umri wa miaka 31.

Wilshere alistaafu kucheza mwaka jana lakini ameanza vyema maisha yake ya ukocha, na kukiongoza kikosi cha Arsenal chini ya umri wa miaka 18 kutinga fainali ya Kombe la FA katika msimu wake wa kwanza.

Vyanzo viliambia ESPN Wilshere anafuraha Arsenal, lakini ana nia ya kuhamia katika nafasi ya usimamizi wa juu zaidi na sasa anasubiri kusikiliza ofa ya klabu hiyo ya MLS.

The Rapids kwa sasa wako mkiani mwa Ligi ya Ukanda wa Magharibi ya MLS baada ya kuachana na kocha mkuu, Robin Fraser mwezi uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live