Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jack Grealish: Silva usiondoke Man City

Grealish Vs Silva Jack Grealish: Silva usiondoke Man City

Wed, 14 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Manchester City, Jack Grealish amejirekodi video akimtaka kiungo mshambuliaji wa mabingwa hao wa Ulaya, Bernardo Silva asiondike na aendelee kubaki klabuni hapo wapige kazi.

Kiungo huyo Mreno Bernado Silva amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Paris Saint-Germain dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi na tayari ameshawaambia mabosi wa Man City anataka kuondoka.

Silva awali alitaka kwenda Barcelona, lakini miamba hiyo ya Nou Camp bado haipo vizuri kiuchumi na hivyo haitakuwa na pesa inayofaa kunasa huduma ya mchezaji huyo.

Wakati Man City ikifanya paredi ya kushinda mataji matatu msimu huu, Grealish alionekana kwenye video akimwambia Silva: “Tafadhali usiondoke, Bernardo! Tafadhali usiondoke!” Alisema pia kwenye sherehe ya wachezaji hao:

“Ukweli kuna mtu mmoja kwenye hii timu namkubali sana...lakini sasa anaonekana kama mtoto wa mitaani. Jina lake ni Bernardo Silva.” Silva alikuwa na mchango mkubwa kuifikisha Man City fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hatimaye kuichapa Internazionale 1-0 Jumamosi iliyopita na kuwa mabingwa wa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live